WAADIVENTISTI WASEMA: JPM NI MCHA MUNGU WA KWELI. - Mazengo360

Sunday, 3 September 2017

WAADIVENTISTI WASEMA: JPM NI MCHA MUNGU WA KWELI.

ASKOFU MKUU wa madhehebu ya Waadiventisti Wasabato Jimbo la Kusini Tanzania, Mhe Marc Walwa Malakana ametaja Rais John Pombe Magufuli kuwa ndiye mfano wa viongozi waadilifu na wenye hofu ya Mungu ambao bara la Afrika linawahitaji ili kuondoa taswira mbaya iliyopo.

Dr+Jim+Photo

RAIS Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa kusikiliza kwa unyenyekevu neno la shukrani toka kwa mmoja wa waumini wa madhehebu ya Waadiventisti Wasabato wa Kanisa la Magomeni, Jimbo la Kusini Tanzania Dkt Jim Yonazi ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Taasisi ya Magazeti ya Serikali (TSN). Anayeshuhudia katikati ni Askofu Mkuu wa madhehebu hayo Jimbo la Kusini Tanzania, Mhe Marc Walwa Malakana juzi jumamosi jijini Dar es Salaam. (Picha kwa hisani ya mpiga picha wetu).

Hayo yametamkwa mbele ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na Mkewe mbele ya waumini waliohudhuria katika ibada ya sabato siku ya jumamosi iliyopita katika kanisa la Magomeni Mwembe Chai, wilaya ya Kinondoni jijini Dar mara baada ya Rais kujumuika nao katika ibada hiyo.
Askofu Mkuu Malakana alisema, Rais John Magufuli ndiye Yusuf wa sasa (aliyetajwa kwenye Bibilia Takatifu) ambaye watanzania na Bara zima la Afrika waliwahitaji sana ili kuwatoa katika taswira mbaya ya kukosa viongozi waadilifu na wenye hofu ya Mungu.
Askofu Malakana aliendelea kueleza kwa hisia kali kwamba, “uongozi si elimu wala akili nyingi bali ni hekima pamoja hofu ya Mungu mtu apewayo kama zawadi toka kwa Mungu, kupitia Roho wake, alifafanua Askofu Mkuu Malakana.
Aliendelea kusema, “Mataifa mengi yanamwomba Mungu awapate viongozi wenye hofu ya Mungu ili watawale kwa haki, tena wenye kumkiri yeye kwa matendo, na kumtaja moja kwa moja Rais Dkt John Magufuli ndiye haswa wa mfano huo.
Amewataka watazania wote kupokea zawadi hiyo toka kwa Mungu kwa kuishi maisha yenye uadilifu na hofu ya Mungu na kusema zaidi kwamba endapo watashindwa kuishi kiuadilifu, mkono wa sheria utawaelemea na dola itawapeleka vifungoni, alieleza zaidi Askofu Malakana.
Nae Rais Dkt John Magufuli amewashukuru waumini hao pamoja na viongozi wote kwa moyo wao wa uvumilivu na upendo kwake na kusema laikusudia muda mrefu kuwatembelea na kusali nao lakini alitingwa na shughuli zingine.
Rais Dkt Magufuli pia alilishukuru kanisa hilo hapa nchini kwa kuisaidia vizuri serikali kutoa huduma za kijamii kwa watu zikiwamo elimu, afya na malezi bora na kuwaomba waendelee kufanya hivyo.
Rais Dkt Magufuli alishindwa kujizuia furaha yake na kueleza hisia zake jinsi anavyovutiwa na kwaya za wasabato pamoja na ujumbe unaotolewa humo na kuongeza kwamba, kinalenga haswa dhamira ya dhati ya kumtukuza  na kumwabudu Mungu wetu, alisema Dkt Magufuli.
Rais Dkt Magufuli alienda mbali zaidi kwa kueleza namna ya kuwatambua na kuwatofautisha waimbaji wa kwaya za waadiventisti wasabato ikiwamo kwa kuangalia nywele zao ambazo ni tofauti kabisa na waimbaji wa kwaya zingine.
Rais Dkt Magufuli amewaomba wauminihaona watu wote waendelee kumwombea kwani kazi anayoifanya ni ngumu na hivyo inahitajisana maombi ya watu na msaada wa Mungu.
Pia Rais Dkt Magufuli amechangia ujenzi wa kanisa jipya kwa kutoa mchango wake wa mifuko mia nne ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni tano ambazo alizitoa na kumkabidhi Askofu Mkuu Mhe Marc Malakana mbele ya waumini wote.

MWISHO.