HALMASHAURI zote
nchini zimetakiwa kuendeleza na kuyalinda maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya
shughuli za michezo na burudani ili kuhakikisha mipango ya matumizi ya ardhi
katika maeneo yao inazingatiwa.
![]() |
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa
akijibu maswali leo Bubgeni
Mjini
Dodoma.
Wito
huo umetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa
Kilolo Venance Mwamoto lililohoji Serikali imechukua hatua gani kuhusu timu ya
taifa kuendelea kufanya vibaya katika michezo ya Kimataifa.
“Serikali
inaendelea kufanya juhudi za kuendeleza michezo nchini ili kuwa na timu bora za
michezo katika ngazi mbalimbali hasa ngazi ya taifa”amesema Mhe.Anastazia
Aidha
alizitaja juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuendeleza michezo ni pamoja
na kutoa na kuendesha mafunzo ya muda mfupi kwa wataalamu wa michezo wakiwemo
Waalimu na Maafisa michezo kwa ngazi za Wilaya na Mikoa kupitia Baraza la
Michezo la Taifa na Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.
Naibu
Waziri Wambura ameongeza kuwa juhudi nyingine zinazoendelea kufanywa na
Serikali ni kuboresha mazingira ili wadau wa michezo wawekeze Kisayansi katika
michezo kuanzia umri mdogo kwa lengo la kugundua na kukuza vipaji na hatimaye
kupata wachezaj mahiri wa timu za Taifa.
Hatua
nyingine ni kutenga shule mbili maalum za michezo kwa kila Mkoa pamoja na
kuhamasisha wadau kuanzisha shule za aina hiyo, kutoa ushauri elekezi kwa Vyama
vya Michezo wakati wa maandalizi ya timu za Taifa zinazoshiriki kwenye michezo
ya Kimataifa ikiwemo Olimpiki, Michezo ya Afrika na Michezo ya Jumuiya ya
Madola, kuendesha na kuratibu mashindano ya michezo kwa ajili ya wanafunzi wa
Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na michezo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) kwa
kushirikiana na Wizara nyingine.
Kwa
upande wa uwepo wa wachezaji wengi wa Kimataifa wanaochezea timu za hapa
nchini, Naibu Waziri amesema kuna wachezaji 40 wa kigeni wanaocheza mpira
nchini wakati wachezaji wa Kitanzania wanaocheza mpira nje ya nchi idadi yao ni
14 huku akisisitiza kuwa Serikali inaendelea kulifanyia kazi suala hilo ambapo
kuanzia mwezi Julai mwaka huu fedha zimeanza kupelekwa Baraza la Michezo la
Tifa (BMT) ili ziweze kutumika katika kusimamia na kuendeleza michezo nchini.
Akijibu
swali la nyongeza la Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay alilouliza kuhusu
uendelezwaji wa Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti
Boys) ambao walionesha uwezo mkubwa katika mashindano ya Kimataifa mwaka huu,
Naibu Waziri Wambura amesema kuwa hadi sasa vijana hao wanalelewa, kutunzwa na
kuendelezwa katika kituo cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili baadae waweze
kutumika katika timu za wakubwa kwa manufaa ya taifa.
Ili
taifa lifanikiwe katika sekta ya michezo, Wabunge wanawajibu wa kushiriki
kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya michezo katika maeneo yao ikiwemo
uibuaji wa vipaji na ujenzi wa miundombinu kwa kuhamasisha wadau mbalimbali.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment