SERIKALI kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa leseni
kwa vituo 32 vya televisheni hapa nchini ikiwa ni kuongeza muonekano na usiku
katika maeneo mbalimbali ya nchi.
![]() |
Mamalaka ya Udhibiti ya Mawasiliano nchini - TCRA. |
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Martin Alexander
Mtonda Msuha Mbunge wa Mbinga Vijijini ambapo alitaka kujua idadi ya vituo
vinavyorusha matangazo kwa njia ya televisheni na Makampuni yanayomiliki vituo
hivyo.
Aliongeza
kwa kuvitaja vituo hivyo vya Televisheni vilivyosajiliwa nchini kuwa ni pamoja
na Independent Television (ITV), Star Television Channel Ten Television, TBC 1,
TBC 2, East Africa Television (EATV), Agape Television (ATV), C2C Television,
Dar es Salaam Television (DTV), Abood Television, CTN Television, Capital
Television, Clouds TV, VIASAT 1 Television, Sibuka Television, Sokoine
University of Agriculture Television (SUATV) na Tumaini Television.
Vituo
vingine ni Mlimani Television, Tanga City Council Television, Imaan Television,
Morning Star TV, Africa Internet Television Ltd, Uhai Television Limited,
Barmedas TV, Target Television, Tabibu Television, Africa Swahili Television,
Cable and Satellite Consultancy Limited, WRM Television Network, Dira
Television, Parliament Media Trust (Bunge TV), Mahaasin Television.
Aidha
alifafanua kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ndio yenye dhamana ya
kutoa leseni ya maudhui ya utangazaji wa Televisheni za aina mbili ambazo ni
Leseni za maudhui yanayotazamwa bila kulipia na maudhui ya Kulipia.
![]() |
Mitambo ya kurushia matangazo ya Televisheni inayo dhibitiwa na TCRA. |
Alizidi kueleza kuwa leseni hizo zimegawanywa kimasoko ambapo kuna leseni za Kitaifa ambazo zinapaswa kuonekana nchi nzima na leseni za Kimkoa ambazo huruhusiwa kutangaza mikoa 10 ya Tanzania Bara, na leseni za kiwilaya ambazo huonekana Mkoa mmoja.
Mgawanyo
huu wa kimasoko unatoa fursa kwa waombaji kutangaza maeneo wanayochagua
kutokana na uwezo wao wa kifedha na kiundeshaji ambapo maudhui hayo ya bila
kulipia yanapaswa kuonekana kupitia visimbuzi vya Makampuni ya Agape Associates
Limited, Basic Transmission Limited na Star Media (Tanzania) Limited. Visimbuzi
hivyo ni TING, STARTIMES, DIGITEK na CONTINENTAL.
Naibu
Waziri Wambura amevitaja vituo vyenye leseni ya soko la Kitaifa kuwa ni TBC1,
Channel Ten, East Africa Televisheni, Independent Televisheni, Star
Televisheni, Clouds TV na Bunge TV wakati vituo vyenye soko la kimkoa ni TV
Imaan, Agape TV (ATV) na TV1 na vituo vilivyobaki vina soko la kiwilaya.
Aidha,
Kituo cha TBC1 ambacho ni kituo cha Umma kinapatikana bila malipo ya mwezi
kwenye ving’amuzi vyote vya miundombinu iliyosimikwa ardhini na vile
vinavyotumia mitambo ya satelaiti kama vile Azam TV, DSTV na Zuku.
Kituo
cha TBC 1 kinalazimika kuonekana bila malipo kwa mujibu wa masharti ya leseni
za makampuni ya miundombinu ya utangazaji ya ardhini (DTT) na Satellite
(DTH).
Kuhusu
muonekano na wa TBC1 maeneo yote nchini, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa
Serikali kupitia Bunge la Bajeti ya mwaka 2017/2018 imetenga jumla ya Sh.
Bilioni 3 ambazo ni fedha za miradi ili kuboresha muonekano wa matangazo ya
TBC1 nchi nzima.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment