OFISI ya Msajili wa
Hazina imesema kuwa Taasisi na Mashirika ya Umma sasa rasmi kutekeleza mkakati
wa utendaji kazi ili kujiendesha na kutoa gawio kwa Serikali yenye lengo la
kuchochea maendeleo kwa taifa na kuendelea kuboresha huduma bora za kijamii.
Hayo yalisemwa jana Jijini Dar es Salaam na Msajili Mkuu wa Hazina Dkt.Oswad Mashindano wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa utendaji kazi baina ya Msajili wa Hazina na baadhi ya Wenyeviti wa bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini.
“Ofisi
ya Hazina inasimamia Taasisi mbalimbali takribani 265, ni vyema Taasisi hizo
kwa kushirikiana kwa pamoja zikasimamiwa vizuri ili kutoa huduma endelevu na
kuchangia katika uwekezaji wenye tija kwa taifa”,alisema Dkt.Mashindano.
Aidha
alisema kuwa mwaka 2014-2015 Ofisi ya msajili wa hazina walifunga mkataba
naTaasisi na Mashirika ya Umma 71 kati ya 265 ambapo mkataba huo ulilenga
katika maeneo manne ya kiutendaji ambayo ni usimamizi katika rasilimali
fedha , watu, utawala bora na huduma kwa wateja.
![]() |
Baadhi ya Wenyeviti wa Bodi
za Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali pamoja Watendaji Wakuu wa taasisi
hizo wakimsikiliza Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (hayupo pichani)
wakati wa hafla ya kuweka saini mikataba ya utendaji kazi kwa taasisi na
Mashirika ya Umma jana jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Mashindano aliongeza kuwa Katika tathmini ya mkataba uliopita kupitia nyaraka
mbalimbali , uchambuzi umeonyesha kuwa zipo baadhi ya dosari katika
utekelezaji wa makubaliano ya awali ambazo alizitaja kuwa asilimia
25 ya mpango mkakati waliojiwekea Taasisi na Mashirika hayaendani
na bajeti waliojiwekea.
Pili
malengo yaliyobainishwa na Taasisis hizo hayaendani na mpango kazi ,
maeneo ya ya usimamizi wa rasilimali watu na utawala bado kuna changamoto, eneo
la ukusanyaji mapato katika baadhi ya Taasisi bado ni ndogo pamoja na
eneo la Huduma kwa wateja linahitaji kusimamiwa ipasavyo na kuwepo kwa baadhi
ya Taasisi na Mashirika ya Umma kujaza matokeo ya kazi ambazo hazipo kwenye
utekelezaji wa mapango kazi.
“Katika
utiaji wa sahihi, mkataba huu unaohusisha zaidi ya Taasisi na Mashirika
30 naamini tutazingatia kutatua changamoto zilizopo na kuweka mpango wa
maendeleo endelevu”, alisisitiza Dkt. Mashindano.
Naye
spika wa bunge mstaafu ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa bima wa
afya Bi. Anna Makinda alitoa neno kwa niaba ya wenyeviti wa Bodi wa
Taasisi na Mashirika ya Umma alisema ni vizuri tukatatua changamoto
zilizojitokeza katika uendeshaji wa mashirika ya Umma ili yajiendeshe kwa tija
na maslahi ya Taifa.
“Watendaji
wakuu wa Taasisi za Umma na wenyeviti wa Bodi tunawajibishwa na makubaliano
haya, tunategemewa sana katika kuwaletea maendeleo wananchi na Taifa kwa
ujumla”, alisema Bi. Makinda.
Aliongeza
kuwa Taasisi za vyuo vikuu vilivyoingia makubaliano haya watawajibika katika
kuwatayarisha vijana katika kuliletea Taifa maendeleo.
Wenyeviti
wa Bodi na watendaji wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma wanatakiwa kufanya
kazi kwa kuzingatia miongozo iliyopo taratibu na Sheria zilizopo kwa
kushirikiana na Ofisi ya Hazina ili kuleta tija kwa watumishi wengine katika
Taasisi za Umma.
Mbali
na majukumu iliyonayo Ofisi ya Msajili wa Hazina pia inasimamia katika masuala
yote ya uwekezaji nchini, mitaji, malipo mbalimbali ikiwemo mishahara kwa
watumishi wa Umma.
Mwisho
No comments:
Post a Comment