POLICE
Mkoani Dodoma imewakamata raia watano wenye asili ya China wilayani Bahi mkoani
Dodoma kwenye eneo kilichopo kiwanda cha kusaga Kokoto cha SANDS Industries Ltd wakiwa na nyara za serekali kinyume cha sheria siku mbili zilizopita.
Pia mtu mmoja mkazi wa
Chang’ombe mkoani Dodoma amekamatwa akiwa na sare za Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ).
Taarifa iliyotolewa na
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma leo, Gilles Muroto imesema nyara
zilizokamatwa ni pamoja na magamba 652 na kucha tano za mnyama aina ya Kakakuona pamoja na
kucha nne na jino moja la Simba.
Kamanda Muroto ameeleza pia
kwamba, aliyekamatwa na sare za jeshi alimtaja kwa jina la Dotto Kapenga,
mwenye umri miaka 43 na alipohojiwa kuhusu uhalali wa umiliki wa sare hizo
hakua na majibu.
Katika operesheni nyingi
Kamada Muroto amesema, polisi mkoani humo inawashikilia watu wengine kumi na mbili
kwa kukutwa na vitu mbalimbali vya wizi kinyume cha sheria.
Amevitaja vitu hivyo vikiwemo
Televisheni kumi na tatu za ukubwa
tofauti, radio mbili aina ya sabwoofer pamoja na deki ya Televisheni moja.
Pia polisi imekamata
printer ya komputa moja, kang’amuzi kimoja pamoja na bangi misokoto kumi na
mbili.
Kamanda Muroto ameeleza
zaidi kwamba, hivi karibuni mkoani Dodoma palizuka wizi wa kutumia bodaboda na
uvunjanji wa madirisha na milango ya ya nyumba za watu,huenda ndiko vitu hivyo
vilikopatikana.
Amewataka watu waliopotolewa
au kuibiwa vifaa vyao vya nyumbani wafike makao makuu ya polisi mkoani Dodoma
kuvitambua vitu vyao.
Aidha Kamanda Muroto ametoa
wito kwa raia wote kuchukua taadhari ya
watu wanaotumia sare za majeshi mbalimbali zikiwemo zile za Jeshi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) au za Polisi na kuwatilia mashaka, watoe taarifa hizo polisi
haraka.
Alipoulizwa taarifa ya
mwendelezo juu ya upelelezi kuhusu kujeruwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki
Tundu Lissu, Kamanda Muroto amesema upelelezi bado unaendelea na wakiwa na
taarifa mpya wataujulisha umma.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment