MKUU
wa
wilaya ya Dodoma Christina Mndeme (pichani) ameibuka mshindi katika uchaguzi wa
CCM ngazi ya wilaya ya Dodoma uliofanyika jana nchini kote.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Christina Mndeme |
DC Mndeme ambaye alikuwa akiomba kuwa mmoja wa wawakilishi watatu wa chama hicho ngazi ya wilaya, kwenye mkutano mkuu wa taifa wa CCM, alijinyakulia jumla ya kura 579 kati ya zote 1127 zilizopigwa kihalali.
DC Mndeme amewashukuru sana
wajumbe wote wa mkutano huo uliomchagua ambapo ameeleza pia kwamba atakuwa
mwakilishi mzuri wa maoni ya wana CCM wenzie katika mikutano ijayo ya chama
ngazi ya taifa.
DC Mndeme amefafafanua pia
kwamba, CCM bado ni chama imara na jamii ya watanzania bado ina imani nacho,
hivyo atashirikiana vyema na wana-CCM wengine kumsaidia Mhe Rais wa Jamhuri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM kutekeleza vyema ilani ya
CCM.
Ameongeza kwamba ushindi
wake umekuja wakati mzuri ambapo yeye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma hivyo
atakisaidia sana chama kuhakikisha serekali inatekeleza vyema mpango wake wa
kuhamia Dodoma kwa ufanisi mkubwa.
Pamoja na kuwepo agizo la Mhe Rais wa Jamhuri Dkt John Pombe
Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM lisemalo, “cheo kimoja mtu
mmoja” Mhe Ndeme ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini kwa hivi sasa.
Aidha, juhudi za makusudi
za kumpata msemaji wa CCM, Humfrey
Polepole ili atoe ufafanuzi juu ya ushindi wa Mhe Christina Mndeme endapo
unakwenda kinyume na agizo la Mhe Dkt Magufuli ama lah, simu yake ya mkononi
ilikuwa ikiita tuu muda wote bila kupokelewa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment