MWISHONI mwa juma staa
wa Tanzania Diamond Platnumz alifanya sherehe tatu za kabla ya sherehe ya siku
ya kuzaliwa, lakini Zari the best day hakuwepo.
Diamond akiwaza yatakayomkuta baadae. |
Sherehe hizo zilihudhuriwa na
'vizito' ndani ya sekta ya Burudani Tanzania, lakini la kushangaza, Zari
hakuhudhuria sherehe hizo huku mbadala wake Hamisa Mobetto akionekana kuingia
kwenye mojawapo wa sherehe hizo.
Msanii staa wa ngoma za Bongo flava
Chibu Dangote almaarufu kama Diamond Platnumz, alisherehekea siku ya kuzaliwa
kwake Jumatatu juma hili Oktoba 2 2017.
Diamond alianza sherehe zake mapema kwa
kuandaa tamasha kubwa za kabla ya siku yake ya kamili ya kuzaliwa siku ya
Ijumaa, Septemba 29 mwaka huu, lakini mazingira yalionyesha wazi kwamba mambo si shwari na mzazi mwenzie the bosslady au Zari.
Diamond akipiga "chabo" simu ya Zari ili aone ana chat na nani. |
Msanii huyo wa kibao maarufu kwa sasa cha 'Hallelujah' aliandaa tamasha la kabla ya siku yake ya kuzaliwa, lililoandaliwa katika Klabu ya Element, iliyopo eneo la Masaki jijini Dar Es Salaam.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment