JAMII TUMIENI FURSA MSAADA WA KISHERIA. - Mazengo360

Breaking

Thursday, 5 October 2017

JAMII TUMIENI FURSA MSAADA WA KISHERIA.

KITUO cha huduma za sheria Zanzibar kimesema licha ya serikali kuifanyia marekebisho sheria ya ushahidi, bado wananchi hawana mwamko wa kushirikina katika kutoa ushahidi ili kurahisisha uendeshaji wa kesi za udhalilishaji kijinsia.
Wanasheria wa Kituo cha Huduma ya Sheria Zanzibar.

Akizungumza katika mafunzo yaliyowashirikisha wananchi wa shehia ya Muyuni C, Afisa mipango wa kituo hicho Ali Haji Hassan amesema hali hiyo imekuwa ikisababisha kuendelea kutokea kwa vitendo hivyo na kuathiri nguvukazi ya taifa.
Amesema zaidi kwamba, ni wajibu wa kila mwanajamii kuachana na tabia ya usiri na kuwafichua wahalifu hao ili kusaidia kutokomeza kabisa vitendo hivyo.
Akina mama wa shehia ya Mayuni C mjini Zanzibar wakiwasikiliza wanasheria walipokutana nao hivi leo. 

Nao wananchi wa shehia hiyo wamesema watahakikisha wanakitumia kituo hicho cha huduma za sheria na mwongozo zaidi pindi wanapokabiliwa na matatizo.
MWISHO.





No comments:

Post a Comment