WAGONJWA WA AFYA YA AKILI WATIWA MOYO. - Mazengo360

Breaking

Thursday, 5 October 2017

WAGONJWA WA AFYA YA AKILI WATIWA MOYO.

RAI imetolewa kwa wataalam wa tiba mbadala ya asili kushirikiana na wizara ya afya Zanzibar ili kusaidiana kupunguza matatizo ya ugonjwa wa akili  nchini.
Daktari Bingwa  wa Magonjwa ya Akili Zanzibar, Hamis Othman akiongea na watafiti wa tiba asili (hawapo) hivi leo.

Rai hiyo imetolewa na daktari bingwa wa magonjwa ya afya ya akili Hamis Othman wakati akihutubia kongamano la wanajumuiya ya utafiti wa tiba asili na mbadala katika hospitali ya magonjwa ya akili iliyoko Kidonge Chekundi, mjini Zanzibar hivi leo.
Daktari huyo bingwa amesema kwamba ushirikiano wa pamoja baina yao utajenga uewelewa zaidi na  kusaidia kutatua matatizo ya wangonjwa hao wa akili  katika jamii.
Amesema zaidi kwamba umoja utapekekea kupunguza changamoto na kusaidia katika matibabu ya wangonjwa hao na kuisaidia pia jamii katika kukabilina na wangonjwa hao.
Watafiti Tiba Asili na Mbadala Zanzibar wakimsikiliza Daktari Bingwa wa magonjwa akili.

Nao wanajumuiya hao wameiomba wizara ya afya kuwatatulia changamoto zinazowakabili ili kuweza kuwa karibu  zaidi na kusaidiana kwa pamoja katika masuala ya matibabu.
 Nae mratibu wa jumuiya ya utafiti na tiba asili na mbadala Zanzibar  (jutijaza) Haji Juma ameshauri kwamba, ni vyema kwa serekali kuwatambua watafiti hao wa tiba asili na mbadala ili kusaidiana nao katika utoaji tiba. 
Kongmano hilo ambalo ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya siku ya afya ya akili  duniani inayoadhimishwa kila mwaka Octoba 10, kauli mbiu ya mwaka huu ni afya ya akili ni sehemu ya kazi.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment