JESHI la
polisi mkoa wa Mjini Magharibi huko Zanzibar linawashilikia watu sita kwa
tuhuma za kuhusishwa na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.
Mitaa ya mji wa Zanzibar. |
Hivi majuzi jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa wengine 20 waliokuwa wakihamsisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir Ali
amewahambia waandishi wa habari kwamba watu hao wamakamatwa katika eneo
la Fuoni Mikarafuuni wakiwa katika sherehe maluum ya vitendo hivyo.
Kamanda Nassir alieleza zaidi kwamba jeshi la polisi
limedhamiriakuongeza msako wa wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ambapo
alisema, vimeanza kukithiri na kupotosha maadili katika jamii.
Aidha, Kamanda Nassir alifafanua zaidi pia kwamba baadhi ya
watuhumiwa hao walifanikiwa kutoroka katika zoezi hilo la ukamataji na hivyo
polisi kufanikiwa kuwakamata watu hao sita tu, usiku wa kuamkia jumapili
iliyopita na kusema zoezi la kuwasaka linaendelea.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment