MAHAKAMA KUU jijini
Dar es Salaam leo imemuhukumu mwigizaji filamu maarufu nchini Elizabeth Maiko au “LULU” kwenda
jela miaka miwili kwa kosa la kuuwa bila kukusudia.
Mwigizaji Filamu maarufu nchini Elizabeth Maiko au LULU. |
Msanii
huyo, Elizabeth alituhumiwa kumuuwa msaani mwenzie marehemu Steven Kanumba mwaka 2012
ambaye inaaminika alikuwa na uhusiano naye ya kimapenzi.
Kwa
mara ya kwanza Elizabeth au Lulu alifikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Aprili 12, 2017, lakini baadaye kesi hiyo ilihamishiwa katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, chini ya Jaji Rumanyika aliyesoma hukumu hiyo leo.
Jaji
Rumanyika amesema, “amemtia hatiani Lulu kwa kosa la kuuwa bila kukusudia kwa
kuzingatia kifungu cha 195 cha sheria” alifafanua zaidi.
Kwa
upande wa Jamhuri ulileta mahakamani mashahidi wanne wakiwemo Seth Bosco ambaye
ni mdogo wake Marehemu Kanumba, waliokuwa wakiishi nae pamoja kwenye nyumba na
marehemu na aliyekuwepo siku ya tukio.
Pia
shahidi mwingine ni Dk. Paplas Kagaiga aliyekuwa Daktari wa familia hiyo ambaye
aliyefika nyumbani kwa Marehemu Kanumba mara baada ya kudondoka wakati wa tukio
hilo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment