ZANZIBAR inatarajia kunuifaka na mradi
mpya wa uanzishwaji wa matumizi ya nishati mbadala ili kuweza kupunguza
uharibufu wa mazingira nchini.
Zanzibar Electricity Corporation. |
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya mpango
wa matumizi ya nishati mbadala mkufunzi wa mradi huo Muhamed
Hassan Khamis kwa niaba ya Katibu Mkuu wizara ya Ardhi, Maji,
Nishati na Mazingira amesema mradi huo upo katika hatua nzuri.
Mkufunzi huyo ameongeza zaidi kwamba ili kuhakikisha
wananchi wa visiwa vya Zanzibar wanafaidika na matumizi ya nishati mbadala
ikiwemo upepo na jua wizara imeona itoe elimu zaidi kwa watu ili kila mmoja
ajue hatua zinazochukuliwa na serekali, alisema.
Amesema “lengo la serekali ni kutoa elimu kwa
wanajamii wote hususani katika maeneo ya vijijini ambako ndiko kunatokea uharibifu
mkubwa wa mazingira” na kuongeza kwamba ndiko kunakochangia mabadiliko ya tabia
ya nchi , alifafanua zaid.
Nae meneja wa mradi huo ambae pia ni Mhandisi
kutoka Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Mohamed Shiraz amesema,
lengo la uanzishwaji wa mradi huo ni kutafuta chanzo kipya cha umeme
kitakachoweza kuisaidia jamii pamoja na kuweka matumizi mazuri ya
nishati.
Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi
wa Nishati Mbadala Zanzibar Methur Matibu amesema, mradi huo pia
unakusudia kupunguza utegemezi wa matumizi ya nishati hiyo kutoka Tanzania bara
na kupunguza pia mzigo kwa serekali ya Zanzibar ili uchumi uwanufaishe zaidi
watu wengi wa Zanzibar.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment