![]() |
Simon Msuva pichani amesema magoli mawili aliyofunga kwenye mechi dhidi yaBotswana yatamsaidia kujiamini katika klabu yake ya Difaa El Jadid pindi atakaporejea Morocco.
Msuva amecheza katika kiwango cha juu dhidi ya Botswana na kufanikiwa kutumia vizuri nafasi alizozipatakupachika mabao yaliyoipa Taifa Stars ushindi wa magoli 2-0 kwenye uwanja wa nyumbani.
“Magoli mawili niliyofunga kwenye timu ya taifa yataniongezea kujiamini na kwenda kufanya vizuri kwenye klabu yangu lakini nitaendelea kuaminika kwenye timu kwa sababu unapocheza kwenye timu ya taifa na kufunga wanaona huyu mchezaji anaweza kutusaidia,” Simon Msuva.
|
![]() |
Taifa Stars ilipata ushindi wa magoli 2-0 mwezi March 25, 2017 katika ushindi ambao imeupata tena leo Septmber 2, 2017 yote ikiwa ni michezo ya kirafiki ndani ya miezi saba.
|
No comments:
Post a Comment